Mkate wa Brown Na Mkate Mweupe Kwa mtu mwenye Kitambi na Kisukari una msaada wowote kiafya?

Jibu ; HAPANA

Ukiuliza Kwa nini Unaacha mkate mweupe unafuata mkate wa brown watakwambia Ule wa brown “Ndio unaoshauliwa Kuliwa maana unakuwa una madini mengi na Kambakamba nyingi”

Hio ndio sababu ya Wengi Kula “Mkate wa Brown na Kupiga Chini Mkate Mweupe”

Sasa “Headlines za Dona Na Brown Bread ziko Ukingoni kupotea” Watu wanakula brown bread sana lakini “Hakuna kupungua,Hakuna Presha kushuka na hakuna Kisukari kupata nafuu”

Kwa nini Hakuna nafuu?

Katika Kitabu changu nimeeleza kwamba Kuna vigezo vikuu viwili vya kupima ubora wa chakula “Glycemic index na Glycemic Load” Rejea Sura ya 21 ukurasa wa 280 kitabu cha SAYANSI YA MAPISHI

Kwamba miaka na miaka tumekuwa tukiambiwa kwamba Sukari huru kama Sucrose (Sukari ya Mezani), Fructose (Kutoka kwenye matunda), nk ndio sukari mbaya lakini Mikate mandazi skonzi keki ugali wali vyenyewe ni vizuri “Kula Bila woga kwa sababu havina mafuta na tukaaminishwa kwamba vina Kalori (vinakupa nguvu) nyingi kuliko vyakula vingine vyovyote”

 

Tizama Jedwali Hili linasema kwamba ” Mkate mweupe gram 30 una GLycemic Load 10 ni sawa na vijiko 3.7 vya Sukari”

Sambamba na Hilo Brown Bread (mkate wa brown) unapokula gram 30 unakuwa na Glycemic Load 9 na vijiko 3.3″

Waswahili wanasema “Maneno Hayo” Kumbe Utofauti wa kukimbilia Brown kuepuka kile kinachopandisha sukari zaidi utofauti wake ni 0.4 tu! ?????

Kumbuka kwamba , Slice moja unayokula wewe huwa ina gram ngapi? Halafu Piga sasa Ina vijiko vingapi? na Unakula Slice ngapi za mkate? Na mwili wako hivi unajua unahitaji sukari kiwango gani kuendelea kujiendesha bila shida miaka na miaka?

Jibu ni kwamba , Mwili wako Una hitaji sukari (Glukosi) kijiko 1 ambapo ni sawa na gram 5 kutembea kwenye Lita 5-7 za damu kwa mtu mzima!

Sasa Wewe unaumiminia mwili Gram ngapi kwa siku? Hivi unajua mwili ukiuzidishia Gram ambazo zinatakiwa zitembee kwenye damu yako mwili unaitikiaje?

Mwili unapo uzidishia Sukari sukari Muda wote unaumiminia sukari tena Nyingi mwili huwa unaitikia kwa kumimina homon inayo tunusuru na sukari kuzidi kwenye damu Insulin! Ambayo Huchukua sukari na kuisukuma kuhufadhiwa katika mfumo wa mafuta na kiwango kidogo Glycogen!

Lakini kadri unavyo Umiminia mwili kiwango kingi Cha sukari Muda wote kwa sababu tunaambiw tule milo 6-8 matokeo yake mwili Unatengeneza “Usugu” Tunaita “Insulin resistance “

Insulin resistance Ni njia moja wapo ya seli ya binadamu kujilinda kwa kutengeneza Ukinzani wa kuitikia wito wa insulin ndani ya damu! Kwa maana hio “Insulin inashindwa kufanya kazi yake ya Kusukuma sukari kuingia ndani ya seli maana seli zimetengeneza ngome kujilinda na sukari unayo mimina!

Dalili kubwa ya Insulin resistance (Usugu wa mwili kwa sababu ya kuurundikia sukari inayopelekea Mafuta mabaya mengi kurundikw kwenye Ini (Non alcoholic Steatosis) ni METABOLIC SYNDROME!

Metabolic Syndrome ni mkusanyiko wa maafa karibia Yote unayo yakua kwamba yanaitwa magonjwa ya lishe kama KITAMBI,KISUKARI,Presha,Upungufu wa nguvu za kiume,Ugumba (PCOS),Mvurugiko wa homoni, Kansa,Pumu nk Kwa pamoja tunaita una “Metabolic Syndrome ” Kwa lugha nyingine mimi watu wenye maradhi hayo yote huwa naita “Ana Kitambi cha Wanga” Wengi huwa wanazani neno kitambi cha wanga ni kile cha nyama uzembe hapana! Sikumaanisha hivyo bali ni “Mkusanyiko wa magonjwa yatokanayo na kuhujumu sukari”

Tafiti zinaonesha kwamba kama Tayari Umeshapata Insulin resistance,Umeshaanza kuteswa na Metabolic syndrome au Kitambi cha Wanga Hakuna faida Yoyote ya Brown bread na Dona labda kama unajifurahisha lakini sio kwmaba “Unataka Chakula kitumike kama tiba”

Ushauri huo utumike kwa watu ambao “hawana Athari za Uhujumu wa sukari na wanga yaani hawana Metabolic Syndrome au Kitambi cha wanga”

Kwa sababu utofauti wa Brown Bread na Mkate mweupe ni Mdogo sana sana!

Ushauri wangu pia, Jamii Ifundishwe vigezo Vingine vikuu vya kuzingatia unapotaka kuchagua chakula kwa kutumia Glycemic index au Glycemic load Bila kusahau insulin index na insulin load Vyote hivi nimevijadili katika kitabu changu ili kila anayesoma apate ukweli wake! Ukitumia Elimu ya Glycemic index yaani uwezo wa chakula flani kupandisha sukari kiwango flani ndani ya muda mfupi, Utakuja kugundua kwamba Mkate wa brown na Mweupe Vinakaribiana sana!

Ushauri mwingine ni kwamba kuna Vyakula vingine vyenye viini lishe Vingi sana na vina nyuzi nyuzi nyingi na sio lazima Ule Wanga na sukari huku ukiwa tayari una Kitambi Kisukari presha Upungufu wa nguvu za kiume una PCOS magonjwa yote hayo kuendelea kumiminia mwili sukari ni sawa na kumpatia Mlevi Bia ukitarajia Pombe itamwishia “Ndio itaendela kukoza kila aongezapo Idadi ya Bia”

Ninaamini kwamba vyakula hivi Vinalevya napenda kutumia neno “Carboholic” tu walevi wa wanga na sukari na Kuviacha vyakula hivi Ili tuondokane na Kitambi kisukari presha imekuwa changamoto”

Ni virahisi sana Kuachishwa “Mayai,Nyama ,Parachichi, Na sio Ugali Wali mikate” Kwa sababu Vyakula vya wanga na sukari vinakevya!

Tatizo Malezi “Haturithi Kitambi na magonjwa ya lishe kutoka kwa wazazi wetu, Ila tunarithishana mapishi na mwenendo mbaya wa lishe katika Ukoo na wote mnajikuta Gene ya Kisukari presha inatembea ukooni kwenu na matokeo yake Gene ya Magonjwa Inajionesha Kwa sababu ya mazingira mabovu ya lishe na mfumo wa maisha”

Ushauri wa “Kula Dona,Kula Brown, Hauwezi kutumika Kuondoa kitambi,Kutibu kisukari na hatimaye dawa zipungue, kwa sababu huwezi kutimia Hio iwe nyenzo ya kuzuia magonjwa Wakati ugonjwa umefikia pabaya”
Ukitakiwa Kupewa Onyo mapema “Kula dona ukiwa mzima, Huwa nasikia na kipimo cha Kula ngumi yako Mapema” Chochote unachoambiwa leo “Kula ngumi yako Ujue ndiye adui anayekufanya Sukari ipande,Uwe kilema,Uwe kipofu,Figo zife zote,Upungufu wa nguvu za kiume ” Vyakula hivyo Viangalie kwa jicho Pevu!

Kwa nyakati hizi Ambazo Tayari umeshaugua Magonjwa ya Lishe Tuache sasa Ngonjera huwa naziita (Maana hazina matunda) Inabaki kumtupia lawama mgonjwa anakosea anakula sana mvivu wa mazoezi! Sasa Tuondoe vyakula ambavyo mwili umeonesha kutokustahimili navyo Jikoni Mwetu Wanga na sukari haijalishi Imekobolewa au haijakibolewa, Mwili hauna uwezo wa kutambua kwmaba Umeupatia chapati lakini unatambua umeupatia “Sukari gram Kadhaa”

-Wanga na sukari Iwe dona au sembe Vyote weka pembeni kitambi cha wanga Kesho kutwa tu kitaanza kutoweka!
-Pata kambakamba Kutoka kwenye Mboga za majani
-Pata nishati kutoka kwenye vyakula Vyenye kukupa nguvu mara dufu, Kama Mafuta asilia
-Ukisha Pungua vizuri Unaweza kuanza mazoezi Polepole kadri mwili wako unavyostahimili

Siku nyingine Tena….Soma Kitabu cha SAYANSI YA MAPISHI kama Tayari unacho Ukurasa No 280

Post a comment

Your email address will not be published.

nine + 15 =

Select the fields to be shown. Others will be hidden. Drag and drop to rearrange the order.
  • Image
  • SKU
  • Rating
  • Price
  • Stock
  • Availability
  • Add to cart
  • Description
  • Content
  • Weight
  • Dimensions
  • Additional information
Click outside to hide the comparison bar
Compare