Siri kwa nini Harmonize Hawezi Kumsamehe Diamond Platnumz ni hii.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Siri kwa nini Harmonize Hawezi Kumsamehe Diamond Platnumz ni hii.


 Siri kwa nini Harmonize Hawezi Kumsamehe Diamond Platnumz ni hii.

Msanii Harmonize kwa mara ya kwanza ametupa mwanga katika aina ya tatizo ambalo limekwamisha kupatikana kwa amani baina yake na aliyekuwa babake katika Sanaa ya muziki, Diamond Platnumz.


Akizungumza kwenye mahojiano na Blogu ya Simulizi na Sauti, msanii huyo pia alikana kuwa hajajaribu kulazimisha urafiki na Hamisa Mobetto – babymama wa Diamond kama njia moja ya kumkomoa Diamond.


Alisema yeye na Hamisa wamekuwa marafiki kwa muda mrefu lakini hakutaka kuliweka lionekana kwamba anamsogelea ili kumkomoa Diamond.


Msanii huyo alisema kwamba katika maisha, kuna matatizo mbalimbali ambayo hutokea kati ya watu, mengine yana wepesi wa kusameheka na kusahaulika lakini mengine pia yanachukua muda kusameheka.


“Unajua kuna vitu viwili, matatizo personal, yaani wewe umekosana na mimi personal, umenitukana au labda umenichukulia mwanamke, nitaamka tu siku moja nikusamehe na yataisha,” alisema.


Lakini je, ni tatizo lipi hili ambalo lilitokea kati yake na Diamond ambalo halijapata kutatuliwa? Harmonize anajibu;


“Lakini pia kuna matatizo ya aina mbili, ambayo yanachukua muda sana kuisha. La kwanza mkiwa mna matatizo yanayohusiana na pesa, kwa sababu hiyo inakuwa kama umeweka kiraka, kila siku nitakavyokuwa na shida nitakuwa nakukumbuka wewe.


"Wewe ukiwa umenidhulumu ama tumepishana kwa mambo ya pesa, nikiwa niko vizuri nitakusahau, lakini nikipata shida tu naona yaani huyu ndiye kasababisha, hiyo inakuwa ngumu sana kuisha,” Harmonize alisema.


Itakumbukwa baada ya kuondoka WCB Wasafi mwishoni mwa 2019, Harmonize alilia sana kwa vyombo vya habari jinsi mkataba wa lebo hiyo ulivyokuwa wa unyonyaji.


Msanii huyo kwa mara ya kwanza alifichua kwamba WCB huchukua asilimia 60 ya mapato ya msanii na kumuachia asilimia 40 pekee.


Zaidi ya hayo, Harmonize alidai kwamba alishurutishwa kuvunja benki yake na kutengana na kima cha milioni 600 za Kitanzania ili kuachiwa huru kazi zake pamoja na kurasa zake za mitandaoni.


Licha ya kufanya hivyo vyote japo kwa kukopa, Harmonize alidai kwamba bado mchakato huo ulicheleweshwa mpaka kupelekea Rais Magufuli (hayati) kipindi hicho kuingilia kati na kusitisha safari ya Diamond kwenda nje ya nchi katika uwanja wa ndege ili kumshurutisha kutia saini ya kumuachia huru Harmonize.


Baadae pia Harmonize alikuja kuibua madai kwamba mapato kutoka kwa ngoma ya Kwangwaru hakuwa anayapokea hata baada ya kulipia usitishwaji wa mkataba na kuachiwa huru kazi zake.


Wengi wanahisi kwamba hili tatizo linalozunguka suala la fedha ndilo limepelekea uhasama wa wawili hao kuendelea kukua na kunenepa hata zaidi kila uchao

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad