You are on page 1of 5

MKATE

WA UNGA WA ALMOND
MAHITAJI
1. Unga wa Dr Boaz KitchenTM almond Flour kikombe 1
2. Mayai 6 yakienyeji
3. Mafuta ya olive oil ½ kikombe kidogo cha chai
4. Baking powder ½ kijiko kikubwa
5. Chumvi yakuonja
6. Dr Boaz KitchenTM Cardamon powder(Iliki) ½ kijiko
7. Maji ya moto au maziwa fresh yakuchanganyia
8. Chombo cha kuchomea mkate (Bread maker)
9. Karatasi nyembamba ya kutanguliza chini kwenye bread make tunaita
baking sheet (Kama huna tumia aluminium foil nyepesi ingawaje ukipata
baking sheet itapendeza zaidi) hii inasaidia mkate wako huwa unatabia ya
kung’ang’ania kwenye kitako utauzuia na umbo lake halite meguka.

HATUA ZA KUFANYA
1. Chukua vitu kwanza vikavu,changanya vyote unga,Chumvi yakawaida tu,
Dr Boaz KitchenTM Cardamon powder(Iliki) na baking poda. Halafu mal-
izia na mayai na vinginevyo. Pasua mayai kwenye bakuli na weka mafuta
yako ya olive oil kisha changanya kwa kutumia hand whisker (Hata kijiko)
2. Hatua ya pili ni kuchanganya vyote kwa pamoja. Halafu sasa tumia maziwa
yako au maji yako kukoroga hadi utakapopata mchanganyiko mzito ongeza
maji kidogo kidogo usije jisahau mchanganyiko wako ukawa mwepesi sana.
3. Baada ya hapo kata kikaratasi cha kuchomea mkate (Vinauzwa madukani
ulizia baking baking paper) tanguliza kwenye kitako cha kifaa chako halafu
weka mchanganyiko wako ili uanze kuchoma.
4. Kama unatumia Oveni pasha oveni yako kwanza kwa dakika 10 nyuzi joto
180 na kisha weka chakula chako choma kwa dakika 45 kwa kutumia moto
ule ule.
5. Baada ya dakika hizo tizama kama mkate wako umeiva hadi ndani chome-
ka kijiti utaona kama kijiti kitatoka kikavu au unyevunyevu kama haujaiva.
6. Baada ya hapo katakata vizuri kabisa kwa kutumia kisu, halafu kama una-
ona haujakauka vizuri weka kwenye oven tena vile vipande kwa dakika 10.
Kama huna oven tumia jiko la kawaida kuoka na bado utapata matokeo
yaleyale.

You might also like