Pata taarifa kuu
AMANI-DIPLOMASIA

Nini maana ya ujumbe wa amani wa Afrika nchini Ukraine?

Ujumbe wa Afrika unatarajiwa Ijumaa hii asubuhi nchini Ukraine. Nchi saba zinawakilishwa na wakuu wanne wa nchi kutoka bara la Afrika ni sehemu ya "ujumbe huu wa amani". Kwenye ajenda: mkutano na Rais wa Ukraine Zelensky na kuzuru Bucha, ambapo jeshi la Urusi linashutumiwa kwa dhuluma dhidi ya raia. Ujumbe huu wa marais kisha utaenda Urusi kukutana kwa mazungumzo na rais wa Urusi Vladimir Putin huko Saint-Petersburg.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ni mmoja wa marais wanne wa Afrika watakaosafiri kwenda Ukraine Ijumaa hii, Juni 16, 2023.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ni mmoja wa marais wanne wa Afrika watakaosafiri kwenda Ukraine Ijumaa hii, Juni 16, 2023. AP - Nardus Engelbrecht
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Comoro Azali Assoumani, Rais wa Senegali Macky Sall, rais wa Zambia Hakainde Hichilema na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pamoja na wawakilishi wa nchi nyingine tatu watawasili leo asubuhi mjini Kiev karibu saa mbili asubuhi, kwa treni maalum kutoka Poland.

Ujumbe huu wa amani ulikuwa na malengo makubwa mwanzoni. Leo, malengo yanaonekana kuwa ya kawaida lakini hasa yako wazi. Mmoja wa wajumbe anakiri kwamba kwanza ni swali la "kusikiliza pande zote mbili, kujua ni shida gani wanaweza kukubaliana na kuanza mazungumzo". Ajenda ni ya kushangaza. Suala la usafirishaji wa nafaka, muhimu kwa Afrika, huenda likajadiliwa. Hasa tangu siku ya Jumanne, Vladimir Putin kwa mara nyingine tena alitishia kujiondoa kwenye makubaliano ya nafaka yaliyohitimishwa mnamo mwezi Julai 2022 ambayo yanahakikisha usafirishaji wake nje ya nchi.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kwa upande wake alisema anaunga mkono ujumbe huo: "Nilipata fursa ya kuwa na rais Cyril Ramaphosa ambaye alinieleza juhudi zitakazofanywa na bila shaka, ninawatia moyo na ninatia moyo juhudi za kuleta amani. Sio juu yangu kufafanua kile watakachoweza kufikia. Nadhani ni muhimu kusisitiza kwamba huu ni mpango muhimu unaozingatia nia njema ya nchi kadhaa ambazo ni muhimu. Bila shaka, ninatumai kuwa katika mazungumzo kati ya Rais Putin na viongozi wa Afrika kutakuwa na matokeo chanya kuhusu Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi, na pia kuhusu juhudi ambazo tunafanya kwa usafirishaji wa chakula na mbolea kutoka Urusi. "

Upeo mdogo

Lakini je, viongozi wa Afrika wataenda mbali zaidi na kuibua ramani ya amani, kama walivyodokeza wiki iliyopita? Kwa hayo yote, bado kiza kinatanda. "Nchi za Kiafrika hazina njia za kushinikiza Ukraine au Urusi. Kufikiria kuwa na uwezo wa kupatanisha ni jambo dogo”, anakariri waziri mmoja kutoka moja ya nchi za Afrika Magharibi.

Majadiliano hayo pia yatakuwa na mstari mwekundu: hakuna suala la kushughulikia masuala ya kijeshi. Wiki moja iliyopita, mkuu wa diplomasia ya Ukraine alisisitiza: “Mpango wowote wa amani lazima uheshimu uadilifu wa eneo la nchi yetu. Hakuna mpango wa amani unaoweza kulenga kusimamisha mzozo,” alisema Dmytro Kuleba.

Kwa kifupi, ni tofauti na maneno ya rais wa Afrika Kusini ambaye, baada ya mkutano wa kawaida wa Juni 5 na viongozi wenzake, aliahidi "kupendekeza vipengele vya usitishaji vita na amani ya kudumu", na kutafuta "dhamira ya kukomesha mzozo.

Hatimaye, marais watatu kati ya nchi saba zilizowakilishwa hawapo, hasa viongozi wenye ushawishi mkubwa kama rais wa Misri Abdel Fatah Al-Sissi. Kwa hiyo wigo wa kisiasa wa mpango huo ni mdogo. Hasa kwa vile mbinu hiyo haikubaliani kwa pamoja katika Afrika. Hivyo, ndani ya AU wanajaribu kujiweka mbali nayo. Chanzo kutoka ndani ya shirika hilo kinasisitiza kuwa ni “kundi la wakuu wa nchi, kwa majina yao wenyewe. Sio misheni ya Umoja wa Afrika Hilo linapaswa kueleweka na kuwekwa wazi. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.