MAPISHI:Mkate wa ndizi

Mkate wa ndizi

KUNA aina mbalimbali za mikate. Mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika utengenezaji wa mikate hiyo.
Katika mapishi leo hii nitakuelekeza namna  ya kutengeneza  mkate wa ndizi. Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa kuna tofauti kubwa baina ya mkate mmoja na mwingine.

Kwa mantiki hiyo, mkate wa ndizi umekuwa na tofauti kubwa ya ladha ukilinganisha na mikate mingine, hasa ukizingatia kuwa huwa na inawekewa viungo tofauti na mikate ya kawaida.

Mahitaji

  • Sukari kikombe kimoja
  • Siagi 1/3 kikombe
  • Mayai mawili
  • Ndizi mbivu zilizomenywa na kusagwa kikombe kimoja na nusu.
  • Maji 1/3
  • Unga  wa ngano kikombe kimoja na nusu cha chai
  • Unga wa soda kijiko kimoja cha chai
  • Chumvi kijiko kimoja cha chai
  • Baking poda robo kijiko cha chai
  • Karanga nusu kikombe cha chai

Namna ya kupika
Changanya sukari na siagi kwenye bakuli moja kubwa la udongo ama plastiki. Hakikisha vinachanganyika kabisa. Kisha weka mayai endelea kukoroga. Halafu unga wa ngano.

Vikishalainika  weka ndizi na saga kwa muda wa dakika tano. Ikiwa unatumia mashine ya kusagia sekunde 30 tu zinatosha kukamilisha zoezi hili.

Chukua viungo vingine vyote vilivyobaki isipokuwa karanga na kisha weka kwenye mchanganyiko wako. Changanya vizuri hadi  vichanganyike vizuri.

Acha mchangayiko wako uumuke kwa muda wa dakika 30. Baada ya hapo mimina katika  bati la kuokea taya ri kwa kuoka. Oka kwa muda wa dakika 30 hadi uwe umei va kabisa .
Baada ya hapo ondoa jikoni weka pembeni.  Acha upoe . Ukishapoa kabisa, katakata silesi

Mkate wako uko tayari kwa kuliwa . Unaweza kula na chai maziwa ama kinywaji chochote kisicho na kilevi.