Mkufu wa dhahabu wapatikana kaburini baada ya maelfu ya miaka  

G

Chanzo cha picha, MOLA

Wanaakiolojia wamegundua mkufu wa dhahabu, uliotengenezwa kati ya mwaka 630-670 AD na kuuelezea kuwa ndio mkufu wenye thamani kubwa zaidi uliowahi kupatikana nchini Uingereza.   

Mkufu huo, uliopatikana karibu na mji wa Northampton,umetengenezwa kwa shilingi ya Waroma, dhahabu na mawe ya thamani.

Una miaka 1,300 na ulipatikana katka kaburi ambalo linadhaniwa kuwa ni mahala alipozikwa mwanamke wa hadhi ya juu, kama vile  kutoka familia kama ya ufalme.   

Wataalamu wameusifu uvumbuzi wa  mkufu huo, wakiuelezea kama uvumbuzi muhimu kwa dunia.   

 Wataalamu kutoka katika makumbusho ya Akiolojia ya London (Mola) waliupata mkufu huo katika eneo la nyumba ya makazi katika Harpole, magharibi mwa   Northampton.

"Tulipoiona dhahabu ikijitokeza kwenye mchanga tulijua kuwa kuna kitu fulani muhimu ," alisema Levente-Bence Balazs,  ambaye aliiongoza timu kutoka Mola.

"Hatahivyo, hatukujua ni umuhimu gani kitu hiki kitakuwa nao.  

G

Chanzo cha picha, MOLA

G

Chanzo cha picha, MOLA

Vikaangio viwili vilivyopambwa na sahani ya shaba pia vilipatikana katika kaburi.   

Hatahivyo, kipimo cha x-ray  cha eneo la mchanga wa kaburi ilifichua kwamba eneo la ndani ya kaburi lilikuwa limepambwa sana. 

Wataalamu wa MOLA wanasema kwamba mwanamke huyu huenda alikuwa ni kiongozi wa dini wa Kikristo.   

G

Chanzo cha picha, MOLA

G

Chanzo cha picha, MOLA

Wataaamu wanasema mifupa yote iliisha isipokuwa vipande vidogo vidogo vya meno.  Hatahivyo, iligundulika kwamba mwanamke wa hadhi ya juu alizikwa katika kaburi lile. 

g

Chanzo cha picha, MOLA

Mikufu kadhaa imekuwa ikipatikana  katika maeneo ya uingereza, lakini hakuna ule unaofanana na huu.

Simon Mortimer, mtaalamu wa vipimo vya udongoa , anasema : "ni kipimo cha mara moja maishani – ni saw ana mambo unayoyasoma vitabuni na sio kitu unachokitarajia kukiona mbele yako."

Mkufu huu utatolewa kama zawadi kwa  taasisi ya utafiti wa udongo ya Soil Resource Center iliyopo  Northamptonshire nchini Uingereza UK.