Kwa nini India haiwezi kutuma jeshi Sri Lanka safari hii kama ilivyokuwa 1987?

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Sri Lanka ilipata uhuru mwaka 1948. Mgororo wa kisiasa na kiuchumi ambao nchi hiyo inapitia leo hii, haujawahi kushuhidiwa tangu ilipopata uhuru.

Hii ndiyo sababu India pia ilituma msaada wa kifedha kwa Sri Lanka, kuchukua hatua za haraka, ikifuata kanuni ya kuwa jirani mwema. 

Wakati huu wa mzozo, watu wengi wanaona usaidizi huu wa kifedha unaofanywa na India hautoshi. 

Mbunge wa zamani wa BJP Rajya Sabha Subramanian Swamy pia ni miongoni mwa viongozi kama hao. 

Anasema kwamba serikali ya India inapaswa kujaribu kusitisha uundwaji wa serikali yoyote isiyo ya kidemokrasia nchini Sri Lanka kwa gharama yoyote.

 

Unaweza pia kusoma

Hoja ya Subramanian Swamy juu ya msaada wa kijeshi

@SWAMY39

Chanzo cha picha, @SWAMY39

Siku ya Alhamisi, Subramanian Swamy alisema katika mahojiano na kituo binafsi cha televisheni cha Kiingereza NewsX, "Rajapaksa na ndugu zake waliingia madarakani kwa kugombea na kushinda. Na leo hii baadhi ya watu wanataka kumng'oa kutoka madarakani. Wanamlazimisha kujiuzulu. Hii ni hali ya hatari sana. Sri Lanka iko kwenye mpaka wa India. Nchi moja ya kisiwa."

"Kuna nchi nyingi ambazo zinapingana na India na zinatafuta fursa. China ni mojawapo, ambayo inaweza pia kusaidiwa na nchi nyingi kama vile Myanmar na Pakistan. India inaliona suala zima kama 'hali ya ghafla'. Nataka India ichukue suala hili zima kama aina ya 'tishio la usalama' na kuchukua hatua ipasavyo."

"Kwa sasa, Rajapaksa wote wawili hawapo tena Sri Lanka. Katika hali kama hiyo, haifai India kupeleka jeshi katika nchi ambayo hakuna serikali." 

Lakini Subramanian Swamy pia anasema kwamba India inapaswa kusitisha uundaji wa serikali yoyote isiyo ya kidemokrasia nchini Sri Lanka kwa msaada wa jeshi lake.

Anaamini kuwa sasa ni wakati mwafaka kwa India kuingia Sri Lanka kwa usaidizi wa Marekani wakati wa kutekeleza mpango wake wa dharura. India inapaswa kujaribu kurejesha amani huko kwa msaada wa Quad, kwa msaada wa Marekani. India ilifanya hivi huko Sri Lanka hapo awali.

SURENDER SANGWAN

Chanzo cha picha, SURENDER SANGWAN

Lini India ilituma vikosi vya kulinda amani Sri Lanka?

Tukio ambalo Subramanian Swamy alikuwa akirejelea ni la mwaka wa 1987.

Mwaka 1987, kikosi cha kulinda amani cha India kilikwenda Sri Lanka kwa madhumuni ya kuweka amani kaskazini mwa nchi hiyo, lakini askari wake wapatao 1,200 waliuawa katika vita na kikosi cha wanamgambo waliotaka kujitenga LTTE.

Lengo la Jeshi la Kulinda Amani la India (IPKF) lilikuwa kuwazuia wapiganaji wa LTTE na kuimarisha amani nchini Sri Lanka. Lakini ndani ya wiki chache vita vilizuka kati ya IPKF na LTTE.

IPKF ilipofika Sri Lanka, Watamil wa Sri Lanka walifikiri kwamba IPKF ilikuwa imekuja kuwalinda, walikaribishwa kwa uchangamfu. 

Watamil ambao wapo wachache nchini Sri Lanka walihisi kwamba Wasinhali walio wengi walikuwa wakijaribu kupunguza ushawishi wa  lugha na dini yao. Uhusiano kati ya pande hizo mbili ulikuwa mbaya.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Sheria yenye utata iliyopitishwa mwaka wa 1956 ikitangaza Sinhala kama lugha pekee ya taifa nchini humo iliwakasirisha wafanyakazi wa Kitamil wanaofanya kazi katika sekta ya serikali kwani ilikuwa ikiathiri kazi zao, kwa sababu hizi, Watamil walianza mchakato wa kutaka kujitenga na nchi hiyo. 

Pia kulikuwa na matukio ya vurugu dhidi ya Watamil, mwaka 1983, wanajeshi 23 waliuawa katika shambulio lililofanywa na LTTE na kusababisha ghasia kote Sri Lanka. Inaaminika kuwa takriban Watamil 3,000 waliuawa katika ghasia hizi. 

Kutokana na hili vita vilizuka kati ya Serikali ya Sri Lanka na LTTE.

Kulikuwa na wasiwasi nchini India kuhusu kutaka jimbo huru la Kitamil Eelam nchini Sri Lanka kwani idadi kubwa ya Watamil waliishi India.

Watamil wengi wa Kihindi waliunga mkono takwa la LTTE kuwa nchi tofauti. Makubaliano yalifikiwa kati ya India na Sri Lanka na saa chache tu baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo Jeshi la Kulinda Amani la India (IPKF) liliondoka kwenda Sri Lanka.

SURENDER SANGWAN

Chanzo cha picha, SURENDER SANGWAN

Watu wengi nchini Sri Lanka walikasirishwa na makubaliano haya. Walihisi kwamba India, nchi kubwa ilikuwa inaingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo ndogo iliyo jirani yake. 

Muda mfupi baada ya kufika Sri Lanka, wanajeshi wa IPKF (Indian Peace Keeping Force) walichukua nafasi ya wanajeshi wa Sri Lanka katika maeneo ya kaskazini. 

Baada ya muda mfupi vita vilizuka kati ya IPKF na LTTE na IPKF ilianza mashambulizi Oktoba 1987 ili kukamata ngome ya LTTE ya Jaffna. Jeshi la India liliitwa tena Machi 1990. 

Wataalamu wengi hata leo wanaita hatua hiyo ya Serikali ya India kama kosa la kihistoria. 

Na wengi wanaingilia mambo ya ndani. Miongoni mwa wale wanaoamini, kuna Profesa Poolapri Balakrishna, ambaye anashikilia vizuri uchumi wa Sri Lanka. Kwa sasa anafundisha katika Chuo Kikuu cha Ashoka, Sonepat.

DDD

Uchambuzi wa Profesa Poolapri Balakrishna

"Uamuzi wa kutuma wanajeshi mwaka 1987 haukuwa sahihi. Tungejaribu kurejesha amani kwa njia ya mazungumzo badala ya kuingilia kijeshi. 

Hili pia lilikuwa kosa kwa mtazamo wa kijeshi kwa sababu jeshi letu lililazimika kupigana katika eneo la msitu ambalo hawakuwa na uzoefu nalo.

Kihistoria pia, mapambano dhidi ya jeshi la msituni hayakuwahi kufanikiwa. Serikali ya Sri Lanka ilishinda vita hivyo kwa sababu pia walishambulia raia kwa mabomu. Serikali ya India haikuweza kufanya hivo. ‘Ndio maana hatukufanikiwa, lakini idadi kubwa ya wanajeshi vijana wa India walipoteza maisha. Ushauri mbaya sana ulitolewa kwa Rajiv Gandhi’. 

Nadhani tumejifunza somo. Sisi sio tu tunasaidia sana wakati huu badala ya kuingia Sri Lanka, lakini tunasaidia watu huko hata kabla hawajaingia barabarani. Mwezi mmoja uliopita, tulitoa msaada wa dola bilioni 3.5. Wakati huu hatua zetu ziko katika mwelekeo sahihi. Sidhani kama jeshi linapaswa kusaidia kwa njia yoyote." 

Je, serikali ya India bado inaweza kusaidia serikali ya Sri Lanka kisiasa?

ggg

Uchambuzi wa Ashok Kanth, mwanadiplomasia wa zamani

"Mgogoro wa kiuchumi wa Sri Lanka kwa sasa tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1948 haujawahi kutokea. India imekuwa ya kwanza kutoa ushirikiano.

India imejitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuisaidia Sri Lanka. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu serikali ya India imetoa mkopo wa dola bilioni 3.8. mbali na hilo, mashirika mengine ya kijamii ikiwa ni pamoja na serikali ya Tamil Nadu yamesaidia Sri Lanka. Tunatuma bidhaa muhimu kama vile mafuta na dawa. Jukumu letu limekuwa chini ya sera ya "Jirani Kwanza" " 

"Pamoja na msukosuko wa kiuchumi, kumekuwa na machafuko huko Sri Lanka kwa njia ya mzozo wa kisiasa. India inaweza kuwa na nafasi ndogo katika hili. India imeweka wazi kuwa tuko pamoja na watu wa Sri Lanka. India ingependa Sri Lanka ipate suluhu ya tatizo hili chini ya katiba ya Sri Lanka na mfumo wa kidemokrasia.

“Wanaozungumza kwamba jeshi lipelekwe ni mambo ya hovyo, India haina sera hiyo, India haitaki hata kuiingilia, tunataka chochote chenye maslahi kwa watu wa Sri Lanka kifanyike." Sri Lanka ni nchi jirani na rafiki, hatutaki machafuko huko lakini suluhu ya mzozo wa kisiasa uliopo itabidi itafutwe na watu wa Sri Lanka.

"Mazingira ya mwaka 1987 yalikuwa tofauti muktadha umebadilika kabisa kwa wakati huu. Mgogoro wa kisiasa uliopo kwa sasa ni suala la ndani la Sri Lanka. Kuhusu mgogoro wa kiuchumi, wanahitaji jumuiya ya kimataifa kuwasaidia. Tumechukua hatua, misaada mingi imetoka India ambayo itaendelea. Lakini pia tunaelewa tofauti kati ya mgogoro wa kiuchumi na mgogoro wa kisiasa.

"Msimamo wa India kuhusu mzozo wa kisiasa uko wazi kabisa kwamba tuko pamoja na watu wa Sri Lanka. Suluhisho la mgogoro wa kisiasa ni kuwatoa nje kupitia mifumo ya kidemokrasia na njia za kikatiba."