Kwa nini ni muhimu kudhibiti hisia hii ili usitapeliwa?

Kwa nini ni muhimu kudhibiti hisia hii ili usitapeliwa?

Karibu rafiki kwenye tafakari yetu ya leo.

Kama ulipitwa na makala iliyotangulia soma hapa

Sifa moja wapo ya watu wenye haiba ya Sangwini ni kuongozwa na hisia badala ya kuongozwa na hisia pamoja na mantiki. Hivyo wanakuwa ni wepesi wa kumwamini mtu kwa haraka zaidi, kuliko haiba nyingine. Hisia ya shauku kwao ni kubwa sana, na inakuwa haina kiasi, hivyo hugeuka kuwa tamaa. Kitu ambacho huwa kinawafanya waendelee kuwa shauku ya kufanya na kukumbatia kila fursa mpya inayokuja kwao. Shauku yao ya kutaka kufanikiwa na kuonekana huwa inawafanya wajikute kwenye matatizo mengi, ikiwemo kutapeliwa na kukubali majukumu bila hata kuyatafakari. Siku za hivi karibuni nilishudia, mtumishi mmoja wa neno la Mungu ninayefahamiana naye akitaka kutapeliwa.  

Tukio la yeye kutaka kutapeliwa lilikuwa hivi; Mtumishi huyu, alidai kuwa ametumiwa zawadi na Mchugaji kutoka Senegal kwa njia ya DHL, lakini ilitakiwa kwanza kulipia milioni moja na laki sita ili zawadi iweze kutumwa kwake. Hivyo rafiki yangu mmoja, kwa kuwa wanafahamiana na wanaukaribu alipewa jukumu la kutafuta hiyo pesa kwa uharaka zaidi. Mtu pekee niliyekuwa naonekana mlengwa wa kuweza kusaidia kutoa hiyo hela ni mimi, hivyo Rafiki yangu alinisihi sana niweze kumsaidia bila kutaja sababu ni nini, Kwani yeye hakuwa vizuri kiuchumi kwa wakati huo.

Niliweka bayana kwamba sina pesa ya kutoa kwenye hilo jambo, hivyo sitaweza kusaidia kwa namna yeyote ile. Pamoja na kwamba pesa nilikuwa nayo, nilikataa kwa sababu nilijua tu huu utakuwa ni utapeli, na pesa hizo hazitarudi ndani ya siku mbili kama alivyo kuwa akiahidi. Baada ya siku tano kupita, sakata la kuombwa pesa liliibuka upya, huku sasa muhusika mwenyewe akifunguka hiyo pesa ni ya nini. 

Hello, Mr. Felician. Bwana Yesu asifiwe sana. Am so sorry kwa ujumbe huu ambao nimekutumia usiku huu lakini ni kwa sababu nahitaji Sana msaada wako katika jambo ambalo limenikabiri kwa sasa. Kunamzigo wangu unatakiwa kutumwa kunifikia huku Tanzania. Na huo mzigo unatumwa kupitia DHL company lakini nahitaji kiasi Cha pesa ili niweze kupata clearlence form kwa ajili ya kupata kibali Cha kuruhusiwa kusafirishwa. Naomba unidhamini katika hili najua Hali ya sasa sio nzuri kwa kila Mtanzania lakini najua kabisa unaweza kunisaidia kunipa dhamana na nikapata mkopo na wiki kesho mi ninakurudishia hiyo pesa kwa sababu ndani ya huo mzigo Kuna kiasi Cha pesa. Naomba unisaidie Sana kuikomboa pesa Yangu na Mungu wa Mbinguni atakubariki. Wako katika Bwana Mtumishi.

Kwa haraka haraka tu nilijua huu ni utapeli wanataka kutapeliwa. Niliingia google na kuandika “scam from Senegal” ambako inasemekana zawadi hii ilikuwa inatumwa kuja Tanzania. Nilikutana na ujumbe kutoka kampuni ya DHL Senegal wakiwaonya watu juu ya utapeli unaotumia nembo na anwani na za DHL kuwaibia watu mtandaoni. 

DHL walienda mbali zaidi kwa kutoa namna barua pepe zao zilivyo tofauti na barua pepe za wezi wa mtandaoni mfano; barua pepe kuto DHL, lazima itakuwa na @dhl.com wakati zile barua pepe za matapeli zitakuwa na kikonyo cha @gmail.com, @yahoo.com au @aol.com. Nilimwambia anitumie ile barua pepe aliyotumiwa kutoka DHL Senegal, na aliponitumia ikuwa na kikonyo cha dhl@aol.com

Hivyo ilikuwa wazi kuwa wale walikuwa ni matapeli wa mtandaoni. Licha ya kuwapa maelezo ya kina na ushaidi kedekede, bado rafiki yangu na Mtumishi yule, walikuwa hawaamini kuwa huo ni utapeli. Waliendelea kunisumbua kwamba niwasaidie kwa hilo, kwani jambo lao hilo lilikuwa ni tofauti kabisa na utapeli mwingine, hivyo wasingetapeliwa. Kwa sababu ya haiba yao ya Sangwini kuwa rahisi kutapeliwa kwa sababu wana tumia hisia sana kuliko fikra waliendelea kuwasiliana na matapeli wale mpaka pale walipokuja kujiridhisha kuwa ule ulikuwa ni utapeli wa mtandaoni. 

Rafiki, kama wewe haiba yako ni Sangwini jua ya kuwa uko katika hatari ya kutapeliwa au utakuwa ulishawahi kutapeliwa. Jambo la muhimu ni kuifahamu haiba yako, lakini pia kuweza kudhibiti na kuzitawala hisia zako, hasa hisia ya shauku. 

Ukawe na siku njema rafiki, unapoendelea kutafakari hisia zetu na umuhimu wake kwenye mahusiano yetu. Pia ili kuendelea kupata makala hizi na huduma zetu kwenye emaili yako jiandikishe hapa chini.

Felician Meza

Mwandishi wa vitabu,

Mwalimu wa mafanikio

Mwanasayansi

© Felician Meza 2021

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *