top of page

Mkate wa Mchele

Mchele vikombw 2

hamira vijiko 2 vidogo

Hiliki kiasi upendavo

ute wa yai moja

sukari kiasi upendacho

Tui la nazi kikombe 11/2

Maelezo:

1: Roeka mchele usiku mzima

2: kesho yake, uchuje mchele vizuri utoke maji yote

3: Weka mchele,hiliki,hamira,sukari,ute wa yai na tui lako la nazi kwenye blenda.

4: Saga vitu vyote kwa pamoja mpaka mchele usagike vizuri

5: weka uji wako kwenye bakuli na ufunikie vizuri

6: weka bakuli ya uji kwenye pahali pajoto ili uji wako upate kuumka vizuri

7:Ukisha uumuka, chukua chombo chako cha kuchomea na ukipakaze mafuta kidogo kisha umimine uji wako wa mkate.

8: Weka kwenye oven na uchome kwa moto 150-200

9: ukishaiva uweke kando na uupake mafuta kidogo kwa juu (si lazima)

10: Ufunikie na uuwache upoe

Na ukisha poa unaukatakata vipande upendavo na makate wako utakua tayari kwa kuliwa


bottom of page