COVID 19 - Our shipping update Read more *Important.

Vitu 7 msingi vya nywele kila mwanadada kua navyo.

Vitu 7 msingi vya nywele kila mwanadada kua navyo.

Mambo ndugu yangu,

ni muda kidogo na nimewa miss!!!…. tumeamua blog iwe kwa lugha ya Kiswahili manake si unajua maudhui ni machache kwa lugha yetu wenyewe na instagram yetu kingereza mno! Well we are embracing it! ntatupia kizungu hapa na pale nikishindwa kutafsiri lol!. .

 

Wanawake tunasifiwa tunapo onekana tumependeza muda wote licha ya majukumu 1000 tulionayo..ila unapata wapi muda wa kusoma kila kitu? kuangalia na kujifunza kila kitu? well… nimebahatika kua miongoni mwa watu wanaosifiwa sana kila nnapo suka kitu na ninashukuru mungu kwa hilo. Ambalo watu hawatambui ni kwamba mimi ni mtundu sana..lakini ntaweka wazi kila kitu nnachokifanya binafsi.

unaweza kutazama picha zangu hapa kwenye akaunti yangu binafsi ya Instagram, 99% huwa nimesukia nywele zetu za Kimz

Orodha ofcourse ni ndefu. ila kuna vile vitu ambayo naona ni vya msingi zaidi kua navyo, nina kuhakikishia kwamba afya ya nywele yako itabadilika, kupendeza kutazidi kikomo na utajikuta unasifiwa kutwa na hela ume save. Kigezo cha kusema vitu hivi ni vya msingi tumefanya kwa kuangalia

-Kama ni kizuri kwa afya ya nywele.

– mitindo inayopendwa na wanadada au wamama na

– vitu vitakavyotumika kutunza mitindo hii yote.

Makundi ya Kigezo cha pili ni:( yaani hivi vifaa vinatumika kwenye makundi yote haya)

1. Crochet na weaving.

2. Rasta,locs na twists,

3.mawigi na vibanio

4.kubana natural hair,

5.kubana nywele zenye dawa.

ORODHA YENYWE.

1. Shampoo isio na kemikali kama – sulphates na Parabens.

sulphate ni ile kemikali inayofanya shampoo yako ikichanganywa na maji iwe na povu, hii husaidia shampoo nyingi isitumike na nywele hutakata. changamoto ya sulphate ni kua inaondoa mafuta yote kwenye nywele na ngozi yanayohitajika na pia inaweza kufanya ngozi iwashe, iwe nyekundu haswa kwa watu wenye ngozi sensitive.

Parabens: ni kihifadhi kwenye bidhaa za urembo kinachosaidia zikae muda mrefu bila kuharibika. Lakini kuna tafiti zimeonesha kuwa baadhi ya aina ya kihifadhi hiki kuwa na uwezo wa kuingia ndani ya ngozi. Tafiti pia zinaonesha kuna kiasi chake kimeonakana kwenye tishu za matiti ya wanawake waliogundulika kuwa na saratani ya matiti na inasadikika ni moja wa chanzo cha saratani na matatizo ya uzazi kwa wanawake. Kama precaution makampuni mengi yameitikia wito na kutoweka parabens na sulphate kwenye bidhaa za nywele na za urembo.

Trust me,

1. Ni muhimu kuwa na chupa walau moja moja ya shampoo na condtioner nyumbani, hata kama unapendelea kusafisha nywele yako saluni. Kuna wakati inashindikana, mfano; Ukitoka kwenye mihangaiko yako au gym, na umetoka na jasho lingi, its Nice uweze kuzisafisha ngozi na nywele siku hio badala ya kungojea wiki 2 nywele zichakae ndo uende saluni. Ukuaji wa nywele hutegemea sana afya ya ngozi ya nywele. Ili zikue ni muhimu sana ngozi ya kichwani iwe safi na isiwe kavu muda mwingi. Ukiongeza mafuta kwenye ngozi chafu ndio mwanzo wa kuijaza zaidi uchafu, Chawa na bacteria mbalimbali wana uwezo wa kuzaliana, muwasho unaoweza kupelekea kuchubuka kwa ngozi n.k. chukua muda kujisafisha ngozi hata kama umesuka crochet, Locs, rasta n.k kadiri ya mahitaji ya afya ya ngozi yako hata kama ni baada ya siku tatu.

Shampoo hii imetengenezwa hapa hapa Tanzania, haina kemikali zozote. Inunue hapa
2. Leave – in – conditioner.

Wengi wetu tuna hangaika na nywele zetu ili zikue, zirefuke, zijae na zipendeze. Afya ya nywele huchangiwa na afya zetu, afya ya ngozi ya nywele na nywele yenyewe. sasa ukisha safisha nywele mara nyingi unakua umeondoa mafuta karibia yote kwenye nywele. kwa hio ni muhimu kurudisha mafuta haya, hapa ndipo leave- in- conditioner inapokuja. Itaipa nywele yako unyevu na nyingine kurudisha pH ya nywele yako vizuri (4.5-5.0) bacteria na wadudu wengine wasiishi na kuzaliana kwenye ngozi.

BONUS TIP: unaposuka mitindo kama crochet, ukichanganya vijiko vidogo viwili vya leave-in- conditioner pamoja na maji kwenye chupa ya kupulizia (spray bottle) unapata mafuta mazuri unayoweza kutumia kuchambulia nywele, kutenganisha mawimbi, kupulizia locs au rasta au msuko wako wowote mara chache kwa wiki ziendelee kupata unyevu, also una uwezo wa kupulizia msuko wako kabla ya kufumua ili rasta zitoke kwa urahisi zaidi na nywele isikatike. Una weza kutumia kwenye mawigi yako na pia hata kwenye nywele zako zenye dawa. Kwahio hio ndo yatakaua mafuta yako ukisuka mtindo. .5 stars ! ding ding ding…

Hii binafsi ni hands down moja ya Leave-in conditioner nzuri DUNIANI. My favourite! na inatengenezwa hapa hapa Tanzania. Inunue hapa
3. Chupio

Ni kitu kidogo na tena cha bei rahisi sana ila wanawake wengi sana hawana nyumbani. Ikija kwenye kubana nywele zako halisia, chupio ina uwezo wa kubadilisha sana muonekano wako haswa nywele fupi. Styles ziko nyingi sana..infact, unaweza kutumia kuficha ncha za nywele zako ili zisikatike kirahisi..labda nitafanya video  IGTV yetu kuonesha hii.

Ikija kwenye crochet ndo usiseme. nywele nyingi za crochet unapotoka tu kusuka zinakua zimetuna kwa sababu zimetoka tu kuchambuliwa ila hurudi baada ya siku chache. Sasa kwa zile ziku chache za mwanzo unafanyaje? chupio ndugu yangu! nyanyua nywele za kwenye way, bana na chupio palipo tuna kama kwenye picha ya chini hapa na kisha achia nywele za kwenye way. utabadilika hadi utashangaa, nywele zikisha nywea vizuri ondoa chupio na ufurahie mtindo wako kama kawaida. Ikija kwenye vibanio vya kupachika, chupio inatumika balaa.. uitumie kukiweka kibanio chako kama unavyotaka.. kutawanya nywele au kuzileta pamoja,kushindilia au kuonganisha na kadhalika. Rahisisha maisha yako, nunua zako tu seti nzima ya chupio na kaa nayo kwenye drawer. comment chini kama ungependa kuona namna nyingi chupio zinarahisisha maisha.

 

chupio zinaweza kutumika kama urembo pia.
zinaweza kutumika pia kama urembo ukizipangilia vizuri.

 

4. Kipande cha stocking kutengenza vibanio vyako vya kuzungusha.

Umeshtuka kidogo? mbona ni kitu kitakacho badilisha maisha yako! bila hata kuingia gharama ya ziada, kama una stocking yako ya zamani, ya watoto au wadogo zako ambazo zimeshawaruka.. unaweza kutengeneza kibanio cha kuvutika unachoweza kutumia kwenye nywele zako natural, nywele zako za rasta, crochet , kabla ya kabana ponytails n.k.

Binafsi ninapendelea kutumia stockings kwa sababu ni laini, rahisi kuvaa na haswa rahisi kutoa. vibanio vinapokua vyembamba sana, vinene sana, hamna urahisi wa kufungua so vinasumbua zaidi. Pia stockings ni kitu ambacho unaweza kutoa vibanio vingi kutoka kwenye nguo moja hivo hata kimoja ukipoteza, una uhakika wa kutoa kibanio kingine. Kikubwa kwenye vibanio ni viwe vinavutika vizuri na kutoka kirahisi bila kukata nywele.

Tunaisadia dunia kama tukitafuta matumizi mengine ya nguo hizi badala ya kutupilia mbali. jifunze hapa kutengenza chako

5. Kofia, Foronya au kitambaa cha silk au satin.

Kuna wimbi kubwa la kutumia kofia za kulalia zilizo tengenezwa na kitambaa cha satin. Kama hukujua, Silk ni material laini na nyororo na satin ni material laini ambazo unapolalia huzuia unyevu kutoka kwenye nywele kuenda kwenye mto au mashuka hivo kuacha nywele zako kavu. Pia unapotumia kofia au foronya hizi sio nywele tu zinanufaika bali hata ngozi yako inaepukana na mikunjamano na alama za kuzeeka mapema. Material ya silk inatengenezwa kwa protein ambazo zinatokana na wadudu kwenye mti wa mulbery na hivyo pia kuipa faida ngozi vile vile ukiacha tu ulinzi wake.

Kwa nywele? unapotumia material hizi kwa crochet yako, kwa vile ni laini inapunguza sana nywele kusuguana, mawimbi kuchambuka zaidi na “Frizz”, hii ni ile hali ukilala ukiamka una vinywele havijatulia vinafanya nywele kufungana zaidi. Hii ambapo ni tofauti ukilalia material ya cotton ambapo the opposite is true.

Kwa rasta, twists na locs, binafsi zinanipunguzia maumivu usiku nikilala nikigeuka nalalia nywele nazivuta then naumia. Pia nina amini hata ukisuka rasta kuna nywele zetu chache zinakua exposed na cotton au vitambaa aina nyingine vitanyonya unyevu mdogo uliopo badala ya kuuacha hapo hapo.

Unaposhindwa kuvaa kofia jitahidi kununua au kushonesha foronya zenye kitambaa cha silk au satin.

Kofia zetu zina kitambaa cha kitenge kwa nje na satin kwa ndani, pia tuna kofia satin lined peke yake. Unapata kwa Tsh.20,000/= Tu.
6. Scissors

Hiki kifaa kiko under-rated vibaya sana. Hakipewi kiki ya kutosha yani! Nina msihi kila mwanamke leo aende dukani atafute mkasi mmoja wa kawaida wa kuweka kwenye dressing table au kimkasi kidogo ile kimoja cha kuenea kwenye pochi.

Changamoto ya nywele ni kwamba zinavutika, zinakatika vibaya (split) na zina fungana na ni kawaida sema tu haipendezi. Ni rahisi kama una kimkasi chako ku trim nywele unayoona imekatika vibaya. Na kwenye crochet yaani ndio usisme. Una hitaji mkasi ku detangle na ku trim ncha zilizochoka kila baada ya siku chache ili nywele zibaki fresh kwa chini. Jamani ukitia maanani mambo haya utashangaa jinsi utaka vyo save hela manake ni kwamba utadumu na mtindo wako muda na mpaka siku unafumua nywele bado unasifiwa huko kichwani na unaulizwa ni nini cha ziada umefanya.

well kama unawaza jamani “nianzie wapi?”  “ninunue nini kwanza?” safari yangu ya kutunza nywele zangu vizuri? Ninakuhakikishia ni hapa anzia! kama tu unapenda na kujali nywele zako, natural au una dawa au dreadlocs..anza hapa (wazungu wanaongezea PERIOD!) Its a good & healthy start. Na hapa sio kwa kuishia jamani… bado kuna vitu amazing ambavyo ukiwa navyo unakua umepiga hatua kubwa zaidi na mimi ntakushauri kadiri ya uwezo wangu. Ningependa kuongezea kua mimi sio daktari.. kwa ushauri wa kitaalam nakuomba umwone daktari ndugu yangu.. hii tunaiita “accepted wisdom ”. Tulisema hii list ina vitu 7, lakini tumeishia sita… nenda kwenye account yetu  Instagram na utakuta kuna Bonus tip ya 7! Tunaomba uache mapenzi tele kwenye post hii na pia uwatumie uwapendao ili wajifunze viwili vitatu.

Mapendo Tele Fam!

-Nice-

 

 

LEAVE A COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *