Vifaa:
- Unga mweupe wa ngano – vikombe 3
- Sukari – 1/3 mug
- Maji – 3/4 Mug
- Maziwa ya unga – 1/2 mug
- Mafuta ya kula – 1/4 mug
- Mtindi – kijiko kimoja cha chakula
- Hamira ( instant) – viijiko 2 vya chakula
- Mayai – 1
- Hiliki.
Namna ya kupika:
- Koroga maziwa ya unga na maji
- Menya hiliki na uziponde.
- Kama unatumia hamira ya chenga weka katika kikombe kidogo, tia na sukari na maji iumke (weka pembeni)
- Kama unatumia hamira ya unga (instant) changanya na unga moja kwa moja
- Chukua unga, weka amira iliyoumuka au instant, weka hiliki, halafu kanda mpaka unga uwe laini.
- Unga ukilainika ufunike kwa muda mpaka uumuke.
- Pakaza siagi katika kifaa (trey) utachotumia kuokea.
- Chukua mchanganyiko na uukate kwa size ya madonge upendayo, kisha weka katika trey ya kuokea.
- Kabla hujaweka kwenye oven, funika trey yenye madonge kwa muda ili yaumuke.
- Weka katika Oven yenye nyuzi joto 150 kwa dakika 15 mpaka igeuke rangi ya brown.
- Ikiiva toa kwenye oven kwa ajili ya kula.