Thursday, April 13, 2017

TAMBUA AINA YA NYWELE ZAKO NA JINSI YA KUZITUNZA

JE UNAJUA MANA YA POROSITY YA NYWELE?
Kwa kawaida ukiangalia nywele za watu weusi karibia zote zinafanana kwa kuangalia kwa macho ila kwa ki utalam zinatofautiana


porosity ya nywele,
 ni uwezo wa nywele kunyonya na kupoteza unyevu na kila mtu ana uwezo wa kutambua nywele zake zina porosity ya aina gani kwa kutumia kipimo rahisi tu.

**Kuna watu wanalalamika mbona nywele zangu hazikui au zinakatika wakati natumia mafuta kama ya fulani.  Ukitaka kujua sababu ndio hizi hapa kwamba nywele zetu zinatofautiana hivyo mafuta fulani yanaweza kukubali nywele za mwenzio na yakakataa kwako

hizo unazoona ndani ya glass ni nywele moja moja. na hivi ndivyo unavyopima porosity ya nywele zako. Hakikisha nywele zako zimeoshwa vizuri hazina mafuta yoyote kisha chukua nywele moja ( hata iliyokatikia
wakati unaosha inafaa cha msingi iwe safi). Iweke kwenye glass ya maji safi kisha subiri kama dakika moja. ukiona imebaki ju kwa muda wote uliosubiri ujue una low porosity ikiwa kati kati ni nornmal na ikishuka hadi chini ni high.

LOW POROSITY
inamanisha nywele zako hazina uwezo mkubwa wa kuingiza/kunyonya unyevu na kutoa kwa haraka. yani unaweza kupaka mafuta yakaka muda mrefu hata ukitembea kwenye upepo yanakuwa yapo tu. Pia ukiosha nywele zinakawia kulowa haraka (kunyonya maji haraka mpaka usugue kidogo ndio yaingie ndani)
-nywele za aina hii zinakuwa zinafungana sana na hazikui haraka kwa sababu ya kutonyonya unyevu wa kutosha. Ni rahisi pia kuweka mba mana mafuta au conditional vinaka muda mrefu kwenye nywele

CHA KUFANYA
usike mafuta mazito kwenye nywele na pia conditional hutakiwi kuweka mara kwa mara. kama umeosha na kuweka conditional ile ya kuosha hakikisha unafunga nywele zako na kofia za plasic au hata mifuko na kama uko na steamer unaweza kuitumia ili ipate joto na kuyeyuka kwa kuweza kupenya kwenye nywele. Osha nywele zako angalau mara moja kwa wek ili kuzifanya zifunguke na kunyonya unyevu kwa haraka(ukiziosha mafuta yaliyoshindwa kupenya yataondoka na zitapumua)

HIGH POROSITY
hawa nywele zao zinaingiza unyevu na kutoa kwa kiasi kikubwa sana. kama umepaka mafuta zinaonekana zimeng'ara kwa mafuta lakini bada ya muda unaona tena ni kavu.

SABABU ZA KUWA HIVYO
mara nyingi nywele ambazo zinawekwa relaxer zinakuwa na high porosity au mtu anayezifuta iwe kwa kubana kwa kukaza sana au kusuka misuko inayokaza sana kiasi kwamba ile hali ya kuvutika kwa nywele inalegea(nywele ukivuta inaonekana kama lastiki sasa unapozivuta kila siku lastiki inalegea

CHA KUFANYA
paka mafuta mazito yanayozifanya zisiwe nyepesi sana na yanayoka muda ili yasipote haraka. ikiwezekana paka hata mara mbili kwa siku . punguza kuzibana au kuzichana kila mara


hizo hapo ju ni mfano wa nywele. hiyo inaonekana ni nywele moja na ndivyo nywele zetu zilivyo ukiangalia kwa macho huwezi kujua kama zinakuwa magamba kama ya samaki (nywele moja ukiiangalia ki utalam ndio iko hivyo)

hiyo ya kwanza inaonyesha low porosity inaonekana magamba yake yamefunika sana na ndio mana ni vigumu kuingiza na kupoteza unyevu kwa haraka. nywele ya pili inaonekana ya kati yani haijafunga sana wala kubana sana hivyo unyevu unaweza kuingia na kutoka kwa kiasi cha kawaida tu. Za mwisho nywele inaonekana magamba yake yako wazi na ndio mana ni rahisi kuingiza na kupoteza unyevu haraka ( watu mnaoweka relaxer mjue nywele zenu zinafunuka hivyo na ndio mana ni rahisi kukatika). Kawaida nywele ukivuta inaonekana kama lastiki yani inavutika lakini unapoivuta sana au kuweka relaxer ile lastiki inalegea au kuisha kabisa na hapo ndio unazifanya nywele zako ziwe rahisi kukatika

**kama unaweka relaxer hakikisha unaritachi kila bada ya wek nane au zaidi mana nywele zinazoota kwa muda huo ni inch moja au wakati mwingine haifiki hana inch moja na ndio inayotakiwa tu kuwekwa dawa na sio ambazo tayari zina dawa. Pia punguza moto kwenye nywele sio kila ukiosha unaenda salon kwenye ma driyer, unaweza kuosha nywele zako nyumbani kisha unazipaka mafuta au leave in conditional, zikaushe na taulo halafu zifunge mabutu kesho yake zimekauka fungua mabutu paka mafuta kisha chana














No comments:

Post a Comment