Jenga msingi

Kama mzazi au mlezi, unajua kinachoifaa familia yako na njia bora zaidi ya kuwafunza watoto wako. Kusaidia familia yako kutumia teknolojia mpya, vifaa na huduma katika ulimwengu wa mtandao unaobadilika kila uchao, kupata ushauri ulio rahisi kutekeleza husaidia. Ndio maana sisi huzungumza na wataalamu wa usalama, wazazi, walimu na jumuiya mbalimbali duniani kote kila wakati - ili kufahamu kinachofanya kazi. Pamoja, tunaweza kusaidia kulea jumuia ya raia wema wa kiteknolojia wanaowajibika.

 • Mambo msingi kuhusu usalama wa familia

  Kwa wazazi walio na shughuli nyingi, pata mapendekezo ya haraka yanayosaidia kuweka familia yako salama mtandaoni.

  Endelea kusoma

 • Weka data yako salama

  Pata vidokezo vichache rahisi vya usalama mtandaoni ili vikusaidie wewe na familia yako kukaa salama mtandaoni.

  Endelea kusoma

 • Kuwa salama popote ulipo

  Jifunze jinsi ya kuzungumza na familia yako kuhusu vifaa vya mkononi.

  Endelea kusoma

Zana za usalama

Gundua vipengele 5 maarufu vya usalama vya Google vilivyoundwa ili kuweka familia yako salama mtandaoni.

Google Play

Tumia udhibiti wa wazazi kuchuja programu kulingana na daraja la maudhui

Unaweza kutumia udhibiti wa wazazi kudhibiti maudhui yanayoweza kupakuliwa au kununuliwa kwenye Google Play. Hii husaidia kupata maudhui yanayokufaa wewe na familia yako.

Pata maelezo zaidi

Fungua Duka la Google Play kwenye kifaa chako.

Kwenye kona ya kushoto upande wa juu, gonga aikoni ya Menyu.

Gonga Mipangilio.

Gonga Udhibiti wa wazazi.

Washa Udhibiti wa wazazi.

Unda PIN.

Gusa Programu na Michezo.

Chagua kiwango cha ukomavu.

YouTube

Weka kichujio ili uzuie maudhui yasiyofaa

Kama hungependa kutoona maudhui ya watu wazima au maudhui yaliyo na vikwazo vya umri unapovinjari YouTube, sogeza hadi mwisho wa ukurasa wa YouTube na uwashe Hali ya Usalama. Hali ya Usalama husaidia kuchuja maudhui ambayo huenda yakakera kutoka matokeo ya utafutaji, video zinazohusiana, orodha za kucheza, maonyesho na filamu.

Pata maelezo zaidi

Sogeza hadi mwisho wa ukurasa wa YouTube na ubofye menyu kunjuzi ya "Usalama".

Bofya chaguo la Washa au Zima ili uwashe au uzime Hali ya Usalama.

Ili kufunga mipangilio hii, ingia katika Akaunti yako ya Google.

Ukishaingia katika akaunti, utakuwa na chaguo ya kufunga mipangilio hii.

Chrome

Dhibiti kile ambacho familia yako inaona kwenye Wavuti

Ikiwa unataka kudhibiti tovuti ambazo familia yako inaweza kutembelea kwenye Intaneti unaweza kutumia Watumiaji Wanaosimamiwa katika Google Chrome. Ukiwa na Watumiaji Wanaosimamiwa unaweza kuona kurasa ambazo mtumiaji wako ametembelea na uzuie tovuti ambazo hutaki mtumiaji wako aone.

Pata maelezo zaidi

Ili ongeza mtumiaji anayesimamiwa kwenye Chromebook yako, anza kwenye skrini kuu ya kuingia katika akaunti na ubofye Ongeza mtumiaji.

Upande wa kulia wa skrini, chagua Ongeza mtumiaji anayesimamiwa.

Bofya Ongeza mtumiaji anayesimamiwa.

Ingia kwenye akaunti ambayo itasimamia mtumiaji anayesimamiwa na ubofye Inayofuata.

Chagua jina la mtumiaji, nenosiri, na picha kwa mtumiaji anayesimamiwa. Bofya Inayofuata.

Android

Toa uwezo wa kufikia programu na michezo iliyoidhinishwa pekee

Je, unataka kushiriki kompyuta kibao yako pasipo kushiriki chochote kingine? Kwenye kompyuta vibao za Android zenye toleo la 4.3 na matoleo mengine mapya, unaweza kuunda wasifu wenye vizuizi ambao utadhibiti uwezo wa watumiaji wengine kufikia vipengele na maudhui kwenye kompyuta kibao yako.

Pata maelezo zaidi

Kama ni wewe unayemiliki kompyuta kibao, gusa Mipangilio → Watumiaji → Ongeza mtumiaji au wasifu.

Gusa Wasifu ulio na vizuizi → Wasifu mpya kisha uupe wasifu jina.

Tumia vitufe vya WASHA/ZIMA na mipangilio ili udhibiti ufikiaji kwa vipengele, mipangilio na programu.

Bonyeza kitufe cha kuwasha/kuzima ili urudi kwenye skrini ya kufunga, kisha gusa ikoni ya wasifu mpya.

Ikishawekwa, skrini ya Mwanzo huwa haina chochote. Gusa ikoni ya Programu Zote ili uanze kutumia wasifu mpya.

Angalia zana zingine za usalama