Jinsi Google Wallet hutumia nambari za kadi za mkopo

Google hutumia nambari za kadi za mkopo na kadi za matumizi unazoingiza katika akaunti ya Google Wallet ili kuchakata malipo ya ununuzi kwenye mtandao na nje ya mtandao unaoufanya ukitumia Google Wallet, ikiwa ni pamoja na shughuli za Google Play, na kwa makusudi ya kufuatilia ulaghai. Ilani ya Faragha ya Google Wallet hutoa maelezo ya kina kuhusu jinsi tunavyotumia maelezo ya akaunti ya Google Wallet, ikiwa ni pamoja na maelezo tunayoyakusanya na jinsi tunavyoyashiriki. Tunashiriki tu maelezo ya kibinafsi na wahusika wengine katika hali zilizofafanuliwa katika Ilani ya Faragha ya Wallet. Nambari za kadi za mkopo na kadi za matumizi unazoingiza katika akaunti yako ya Google Wallet zinasimbwa kwa njia fiche na kuhifadhiwa kwenye seva salama katika eneo salama.