Jinsi Google hutumia utambuzi wa ruwaza

Jinsi Google hutumia utambuzi wa ruwaza ili kupata maana ya picha

Kompyuta "hazioni" picha na video kwa njia sawa ambayo watu huona. Unapoangalia picha, unaweza kuona rafiki yako umpendaye amesimama mbele ya nyumba yake. Kwa mtazamo wa kompyuta, picha hiyo moja ni rundo la data ambalo linaweza kutafsiri kama maumbo na maelezo kuhusu uhusiano wa rangi. Ingawa kompyuta haitafanya kama wewe ufanyavyo unapoona picha hiyo, kompyuta inaweza kufunzwa kutambua michoro fulani ya rangi na maumbo. Kwa mfano, kompyuta inaweza kufunzwa kutambua michoro ya kawaida ya maumbo na rangi ambayo inatengeneza picha ya dijitali ya uso. Mchakato huu unajulikana kama ugunduaji wa uso, na ni teknolojia ambayo husaidia Google kulinda faragha yako kwenye huduma kama Street View, ambapo kompyuta hujaribu kugundua na kisha kutia ukungu nyuso za watu ambao wanaweza kuwa wamesimama mtaani wakati gari la Street View linapopita. Ndiyo pia husaidia huduma kama vile Picha za Google+ kupendekeza kwamba uweke lebo kwenye picha au video, kwa kuwa inaonekana kana kwamba kuna uso. Ugunduaji wa uso hautakuambia uso ni wa nani, lakini unaweza kusaidia kutafuta nyuso katika picha zako.

Ukiendelea zaidi kidogo, teknolojia hiyo sawa ya utambuzi wa michoro ambayo inawezesha ugunduaji wa uso inaweza kusaidia kompyuta kuelewa tabia za uso iliyogundua. Kwa mfano, huenda kukawa na michoro fulani ambayo inapendekeza uso ina ndevu au miwani, au kwamba ina sifa kama hizo. Maelezo kama haya yanaweza kutumika kusaidia na vipengele kama upunguzaji wa macho mekundu, au yanaweza kukuruhusu kuangazia vitu kwa kuweka mashurubu au miwani ya jicho moja mahali sawa kwenye uso wako wakati uko katika Hangout.

Zaidi ya teknolojia ya ugunduaji wa uso, Google pia hutumia utambuaji wa uso katika vipengele fulani. Utambuaji wa uso, kama jina linavyopendekeza, unaweza kusaidia kompyuta kulinganisha nyuso zinazojulikana dhidi ya uso mpya na kuona kama kuna ulinganishi au kufanana kunaowezekana. Kwa mfano, utambuaji wa uso huwasaidia watumiaji wa kipengele cha Pata Uso wangu kuona mapendekezo kuhusu nani anawezakuwa anataka kuweka lebo kwenye picha au video amepakia na angependa kushiriki. Soma zaidi kuhusu Pata Uso wangu katika Kituo cha Msaada wa Google+ .

Jinsi Kutafuta kwa Kutamka hufanya kazi

Kutafuta kwa Kutamka hukurusu kutoa ulizo la sauti kwa programu ya mteja wa utafutaji wa Google kwenye kifaa badala ya kucharaza ulizo hilo. Hutumia utambuaji wa ruwaza ili kunukuu maneno yaliyosemwa kuwa matini yaliyoandikwa. Kwa kila ulizo la sauti linalofanywa kwa Kutafuta kwa Kutamka, tunahifadhi lugha, nchi, tamko hilo na mfumo wetu hukisia ni nini kilichosemwa. Data iliyohifadhiwa ya sauti haiwi na Kitambulisho cha Akaunti yako ya Google labda uchague vinginevyo. Hatutumi tamko lolote kwa Google isipokuwa kama umeashiria dhamira ya kutumia kitendaji cha Kutafuta kwa Kutamka (kwa mfano, kubonyeza ikoni ya mikrofoni katika upau wa utafutaji wa haraka au katika kibodi sibayana au kusema "Google" wakati upau wa utafutaji wa haraka unaashiria kwamba kitendaji cha Kutafuta kwa Kutamka kinapatikana). Huwa tunatuma tamko kwa seva za Google ili kutambua kile kilichosemwa na wewe. Tunaweka semi ili kuboresha huduma zetu, ikiwa ni pamoja na kufundisha mfumo ili kutambua vyema zaidi swali sahihi la utafutaji.