Aina za data za eneo zinazotumiwa na Google

Aina tofauti za maelezo ya maeneo zinaweza kutumiwa katika bidhaa mbalimbali za Google.

Maelezo yaliyodokezwa ya eneo ni maelezo ambayo kwa kweli hayatuelezi kifaa chako kiko wapi, lakini huturuhusu kufahamu kama unapendezwa na mahali hapo au kwamba unaweza kuwa mahali hapo. Mfano wa maelezo yaliyodokezwa ya eneo inaweza kuwa utafutaji wa kujiandikia wa mahali fulani. Maelezo yaliyodokezwa ya eneo yanatumiwa kwa njia mbalimbali. Kwa mfano, ukiandika "Eiffel Tower", tunakisia kwamba unaweza kupenda kuona maelezo ya karibu na Paris, na kisha tunaweza kuyatumia kutoa mapendekezo kuhusu maeneo hayo karibu nawe.

Maelezo ya shuguli ya intaneti , kama vile anwani ya IP, kwa kawaida hutolewa kwa mipangilio tofauti kwa kila nchi, kwa hivyo inaweza kutumiwa angalau kutambua nchi ambamo kifaa kifaa chako kiko, na kufanya mambo kama vile kukupa lugha sahihi kwa utafutaji wako. Maelezo haya yanatumwa kama sehemu ya shughuli za kawaida za intaneti.

Baadhi ya bidhaa, kama vile maelekezo ya mgeuko kwa mgeuko katika Ramani za Google za simu, hutumia maelezo sahihi zaidi ya eneo. Kwa bidhaa hizi, kwa kawaida unafaa kuchagua kuwasha huduma za eneo zinazotegemea kifaa, ambazo ni huduma ambazo zinatumia maelezo kama vile ishara za GPS, sensa za kifaa, maeneo ya ufikiaji wa Wi-Fi, na vitambulisho vya minara ya simu ambayo inaweza kutumiwa kupata au kukadiria eneo sahihi. Unaweza baadaye, kuchagua kuzima huduma za eneo zinazotegemea kifaa. Baadhi ya vifaa na/au programu zinaweza pia kukupa mipangilio ya ziada ya kudhibiti eneo kwa huduma hizi za eneo zinazotegemea kifaa. Kwa mfano, katika baadhi ya bidhaa, unaweza kuchagua kama utahifadhi maeneo haya katika bidhaa hiyo au katika historia ya akaunti.