Teknolojia na Kanuni

Hapa Google, tunafuata mawazo na bidhaa zinazopita mipaka ya teknolojia zilizopo. Kama kampuni inayowajibika, tunajitahidi kuhakikisha kuwa uvumbuzi wowote unawiana na kiwango kifaacho cha faragha na usalama kwa watumiaji wetu. Kanuni zetu za Faragha husaidia kuelekeza uamuzi tunaofanya katika kila kiwango cha kampuni yetu, ili kusaidia kuwalinda na kuwawezesha watumiaji wetu tunapotimiza wito wetu unaoendelea wa kupanga maudhui ya ulimwengu.

Kanuni za faragha

 1. Tumia maelezo kuwapa watumiaji wetu bidhaa na huduma zenye manufaa.

  “Lenga kutoa uzoefu bora zaidi kwa watumiaji” ni itikadi ya kwanza ya Falsafa ya Google. Wakati watumiaji wanashiriki maelezo nasi, inatuwezesha kutengeneza huduma na bidhaa ambazo ni za manufaa kwao. Tunaamini kuwa kuzingiatia watumiaji hukuza bidhaa zenyewe na vipengee vinavyolinda faragha ambavyo vimechochea uvumbuzi na kujenga jumuiya wa watumiaji waaminifu kwenye wavuti.

  Tunajifunza kutoka kwa makosa ya kuchapa na makosa ya maendelezo tunayoyafanya sote tunapotafuta ili kukupa matokeo bora ya utafutaji na kwa haraka. Kwa hivyo ukicharaza [simba msrara] tunaweza kukisia ulimaanisha [simba marara].

 2. Kuza bidhaa zinazoonyesha kiwango na desturi thabiti za faragha.

  Azma yetu ni kuwa katika mstari wa mbele wa teknolojia, pamoja na ukuzaji wa zana zinazowasaidia watumiaji kudhibiti maelezo yao ya kibinafsi kwa njia rahisi na ya karibu bila kuondoa manufaa ya uzoefu bora kwa watumiaji. Tunafuata na sheria za faragha, na zaidi ya hayo tunafanya kazi kindani na wasimamizi na washirika katika sekta hii kuweka na kutekeleza viwango thabiti vya faragha.

  Tuliunda Google+ ikiwa na miduara ili kurahisisha kushiriki vitu tofauti na watu tofauti. Kwa hivyo unaweza kuweka marafiki zako katika mduara mmoja, familia yako katika mwingine na bosi katika mduara akiwa pekee yake – kama vile katika maisha halisi.

 3. Fanya ukusanyaji wa maelezo ya kibinafsi uwe wazi.

  Tunajitahidi kuonyesha watumiaji maelezo yanayotumika kuwapa huduma mwafaka zaidi kwao. Inapofaa, tunalenga kuwa na uwazi kuhusu maelezo tuliyo nayo kuhusu watumiaji na jinsi tunavyotumia maelezo hayo kutoa huduma zetu.

  Dashibodi ya Google husaidia kujibu swali, “Google inajua nini kunihusu?” Inakuonyesha maelezo yaliyohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google, kama vile chapisho lako la mwisho kwenye Blogger au picha zako zilizopakiwa, na inakuwezesha kubadilisha mipangilio yako ya faragha kwa bidhaa nyingi za Google kutoka mahali pamoja.

 4. Wape watumiaji chaguo za maana za kulinda faragha yao.

  Watu wana shauku na mahitaji tofauti ya faragha. Kuhudumia watumiaji wetu wote, Google hujitahidi kuwapa chaguo za maana na mahususi juu ya matumizi ya maelezo yao ya kibinafsi. Tunaamini kuwa maelezo ya kibinafsi hayafai kuzuiliwa na tumejitolea kutengeneza bidhaa zinazowaruhusu watumiaji kuhamisha maelezo yao ya kibinafsi kwa huduma zingine. Hatuuzi maelezo ya kibinafsi ya watumiaji.

  Kupitia zana zetu za faragha unaweza kusimba trafiki ya utafutaji kati ya kompyuta yako na Google, kuvinjari wavuti kisiri, kufuta historia yako ya utafutaji na kuhamisha data yako kutoka kwa bidhaa za Google kwa urahishi kupitia juhudi za Ukombozi wa Data, na mengi zaidi.

 5. Kuwa msimazi anayewajibika kwa maelezo tuliyo nayo.

  Tunatambua jukumu letu kulinda data ambayo watumiaji wanatukabidhi. Tunachukulia maswala usalama kwa uzito na tunashirikiana na jamii kubwa ya watumiaji, wasanidi programu na wataalamu wa nje wa usalama ili kufanya Wavuti mahali salama na thabiti zaidi.

  Tunaunda usalama na uthabiti katika bidhaa zetu tangu mwanzo. Zana zetu za ukaguzi wa kiotomatiki hutumia data kuwalinda mamilioni ya watumiaji dhidi ya programu mbaya, mitego ya hadaa, ulaghai na taka kila siku.