Jinsi Google inavyotumia data wakati unatumia tovuti au programu za washirika wetu

Tovuti nyingi hutumia teknolojia za Google kuboresha maudhui yao na kufanya yapatikane bila malipo. Unapotembelea tovuti ambayo inatumia bidhaa zetu za utangazaji (kama AdSense), bidhaa za mitandao ya jamii (kama vile kitufe cha +1) au zana za uchanganuzi (Google Analytics), kivinjari chako cha wavuti hutuma maelezo fulani kwa Google moja kwa moja. Maelezo haya yanajumuisha kwa mfano, anwani ya wavuti ya ukurasa unaotembelea na anwani yako ya IP. Tunaweza pia kuweka vidakuzi kwenye kivinjari chako, au kusoma vidakuzi ambavyo tayari vipo.

Vile vile, programu zinazoshirikiana na Google zinaweza kututumia maelezo kama vile jina la programu na kitambulishi ambacho hutusaidia kubaini matangazo ambayo tumeonyesha katika programu nyingine kwenye kifaa chako. Ikiwa umeingia katika Akaunti ya Google, tunaweza kuyaongeza maelezo hayo kwenye Akaunti yako na kuyachukulia kuwa maelezo ya kibinafsi, kulingana na mipangilio ya Akaunti yako.

Jinsi tunavyotumia maelezo yaliyotumwa na kivinjari chako

Unapotembelea tovuti au kutumia programu zinazotumia teknolojia za Google, tunaweza kutumia maelezo tunayopokea kutoka tovuti na programu hizo kufanya, kwa mfano:

Jinsi unavyoweza kudhibiti maelezo yaliyotumwa kwa Google

Kwa vidokezo na ushauri kuhusu kuwa salama na kusimamia data yako mtandaoni, tembelea Kituo cha Usalama cha Google.

Hizi ni baadhi ya njia unazoweza kudhibiti maelezo yanayoshirikiwa na kivinjari chako cha wavuti unapotembelea au kutumia huduma za Google kwenye tovuti za washirika katika wavuti: